Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Leseni

A AINA TARATIBU 1 Leseni ya Biashara chini ya Sheria ya utoaji leseni za biashara ya No. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya mwaka 2014. Leseni ya kuhuishwa (Renewal) Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuambatanisha kivuli cha leseni iliyoisha muda wake. Leseni Mpya Mwombaji anapaswa kutekeleza yafuatayo:-  Kujaza kikamilifu fomu ya maombi.Kuambatanisha kivuli cha Namba ya usajili wa mlipa kodi (TIN).  Kuambatanisha uthibitisho wa uraia (kivuli cha cheti cha kuzaliwa, Passport ya kusafiria,cheti cha utaifa, kiapo Mahakamani , cheti cha kupiga kura.Uthibitisho wa maandishi eneo la kufanya biashara.Kama ni Kampuni ambatanisha nakala ya cheti cha usajili wa Kampuni na Memorandum and Articles of Association.Kama ni jina la biashara aambatanishe vyeti vya usafili Brela (registration Certificate na Extract from Register) Kwa mwombaji ambaye sio raia wa Tanzania aambatanishe kibali cha kuishi nchini daraja A.Kama wenye Kampuni hawaishi nchini wanawakilishwa , waambatanishe hati ya kiwakili (power of Attorney).Kwa waombaji wa biashara za Kitaalamu waambatanishe vyeti vya kuruhusiwa kufanya biashara hizo kutoka Mamlaka husika.