Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika

Idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika– Halmashauri ya Manispaa ya Temeke 1.0. Utangulizi Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilianza kazi zake mwaka 2013 baada ya kutenganishwa kutoka kwenye iliyokuwa Idara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo. Shughuli za kilimo zinazosimamiwa na idara hii zinachangia 30% ya chakula kutokana na kaya 24,608 ambazo ni sawa na 13% zinazojishughulisha na kilimo kati ya 189,295 zinazoishi pembezoni mwa mji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Kati ya hektari 656,000 za eneo lote la Manispaa ya Temeke  hektari 45,000 zinafaa kwa kilimo na hektari 28,000 ndizo zinazoendelezwa kwa kilimo.