Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

BIASHARA

BIASHARA

Wananchi wa  Wilaya  ya  Temeke kwa  zaidi ya  asilimia (60%) ni watu waliojiajiri  kwenye sekta isiyorasmi.

Shughuli kubwa wanazofanya  ni pamoja  na usindikaji mdogo wa  vyakula, utengenezaji wa  bidhaa mbalimbali kama vile sabuni za  kufulia, dawa  za maji za  kuoshea  vyombo na  sakafu, usukaji, uuzaji wa  mazao ya  kilimo uvuvi na  ufugaji hasa  kwenye  masoko na  magulio.  Wapo baadhi ya  wananchi ambao wameweza kurasimisha  biashara  zao  na  hivyo kuweza kuanzia  viwanda vidogovidogo na vya  kati na  wachache viwanda  vikubwa. Wilaya ya  Temeke inayo zaidi ya  viwanda vidogovidogo 1550 ambavyo vingi ni vya  Useremala, usagaji wa  nafaka, utengenezaji wa vyakula  vya  kuku, kuoka  mikate, kutengeneza nguo hasa  batiki n.k.

Changamoto kubwa  iliyopo kwa  sekta isiyo rasmi pamoja  na  wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wamesharasimisha shughuli zao ni ubora wa  bidhaa wanazotengeneza, ufungaji wa bidhaa, masoko, mtaji wa kuendeleza biashara zao, elimu ya  biashara  na  usafiri.

Katika kukabiliana na  tatizo la ukosefu  wa  masoko hasa kwa  mazao ya  Kilimo mifugo na  uvuvi Wilaya ya  Temeke imeboresha kwa kiasi  kikubwa masoko yake  na  pia  kuanzisha masoko mapya.  Mwaka 2005.  Wilaya ya  Temeke ilikuwa na  masoko kumi na  tano.  Mwaka  2012 idadi imefikia  ishirini na mbili (22) sawa na ongezeko la asilimia  46 Masoko yaliyoanzishwa kwa  kipindi hiki ni Tazara  Veterinary, Rangitatu-Kampochea, Tandika-Kampochea, Makangarawe, Toangoma, Nzasa na  Tundwi Songani.

Masoko ya  Tazara Veterinary, Tandika  (Kampochea) na  Mbagala Rangi tatu (Kampochea) ni maeneo yaliyotengwa rasmi kwa  ajili ya wamachinga kufuatia agizo la Serikali la  kuwapatia  wamachinga  maeneo ya  kufanyia  Biashara.

Kwa  kipindi hiki shughuli zilizofanyika  za kuboresha  masoko pamoja na  ujenzi  wa  masoko mapya ni kama ilivyoonyeshwa kwenye  jedwali hapa  chini.