Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Maelezo mafupi kuhusu Halmashauri

Temeke ni mojawapo ya Halmashauri tatu zinazounda Jiji la Dar es Salaam. Manispaa nyingine ni Ilala na Kinondoni. Manispaa ya Temeke ina eneo la kilometa za mraba 656 na ukanda wa Pwani wa kilometa 70. Aidha ipo katika nyuzi 39012’ – 39033’ Mashariki na nyuzi 6048 – 7033 Kusini. Temeke ipo upande wa kusini mwa Jiji la Dar es Salaam ambapo kwa upande wa Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi, Kusini inapakana na Wilaya ya Mkuranga  Mkoa wa Pwani na upande wa Kaskazini na Magharibi inapakana na Manispaa ya Ilala.

   Hali ya hewa

Kwa ujumla Manispaa ya Temeke ina joto sana katika miezi ya Januari, joto hufikia nyuzi joto 350 na miezi ya Juni hadi Agosti hufikia wastani wa nyuzi joto 250C Halmashauri ya Manispaa ya Temeke hupata misimu miwili ya mvua. Mvua za vuli ambazo hunyesha miezi ya Oktoba hadi Novemba na mvua za Masika ambazo hunyesha miezi ya Februari hadi Mei.