Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Usajili wa Taxi

TARATIBU ZA USAJILI WA TAXI.

A. UTANGULIZI

Magari madogo yanayoshughulika na biashara ya Teksi na (Private hire Vehicles) husajiliwa na sehemu ya bishara  na baadae kupewa namba za usajili chini ya sheria ndogo ya mwaka 1968 (Registaration of Tax Cabs and Private Hire Vehicles) By- Laws 1968.

B. SIFA ZA USAJILI WA TAXI

(A) Rangi nyeupe na mstari wa bluu

(B)Milango minne kwa magari yote

(C) Plate namba nyeupe

(D)  Neon lamp inayofanya kazi

(E)Abiria wasizidi wanne (4) pamoja na dereva

 

C. VIAMBATANISHO

1. Stakabadhi ya malipo ya eneo la Maegesho ya magari lililosajiliwa na Manispaa

2. Kadi ya gari

3. Sticker ya mapato (TRA)

4. License of Tax Cab (income tax)

5. Vehicle inspection report (Traffic Police)

 

D. GHARAMA ZA USAJILI KWA MWAKA

1. Usajili wa gari – 20,000/=

2. Ada ya maegesho – 36,000/=

3. Ada ya kituo – 5,000/=

Jumla kuu ni – 61,000/=

 

E. UKAGUZI WA TEKSI

Baada ya kukamilisha zoezi la usajili wa teksi, ukaguzi hufanyika ili kubaini teksi zote zinazokiuka sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

 

Zinazobainika hutozwa faini ya Tshs.50,000/= kwa kila kosa.

 

Baadhi ya makosa yanayosabisha kukamatwa kwa magari ni:

1. Teksi bubu

2. Teksi zote zisizopigwa rangi maalumu

3. Teksi zisiszokuwa na namba za ubavuni na Neon Lamp

4. Teksi kuegeshwa kwenye eneo lisilorasmi.