Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji

Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji

Majukumu

i. Kuratibu Mipango, Utekelezaji, Usimamizi na tathmini miradi ya Maendeleo katika Wilaya

ii. Kuandaa taarifa za utekelezaji kila robo mwaka ,

iii. Kuandaa taarifa ya Ilani ya Uchaguzi Kila miezi sita

 iv.Kuandaa taarifa za Mafanikio za Serikali iliyoko madarakani

 v. Kuandaa kalenda ya utekelezaji Miradi ya Maendeleo (Action Plan)

 vi.Kuimarisha program ya uwekezaji

         Mafanikio

i. Taarifa mbalimbali za kila robo katika kipindi cha miaka mitano zimeandaliwa na kuwasilishwa katika mamlaka     husika

ii. Mpango Mkakati wa miaka  Mitano umeandaliwa kwa utekelezaji

iii. Mpango wa utekelezaji na Bajeti ya Halmashauri imeweza kuandaliwa kila mwaka

iv. Sera na miongozo mbalimbali ya Serikali imeweza kutafsiriwa na kutekelezwa katika ngazi ya Hamashauri

         Changamoto

i. Ucheleweshwaji wa fedha za miradi ya maendeleo unaopelekea miradi kutokamilika kwa wakati

ii. Ushiriki hafifu wa Wananchi katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo

iii. Wanachi kutotambua umuhimu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo