Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

Afya

Utangulizi.

Huduma za afya katika Manispaa ya Temeke hutolewa kwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wengine kwa maana ya watu na mashirika binafsi (Public Private Partnership) chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke zikisimamiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa.

Katika kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kama zilivyokusudiwa Idara ya afya imegawanyika katika vitengo vikuu 5  ambavyo vinavyofanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba huduma zinazotolewa katika vituo mbalimbali zinakidhi  viwango vilivyowekwa.

Vitengo hivi ni kama ifuatavyo:

1. Uratibu wa Programu za Afya.

2. Uratibu wa Mipango.

3. Utawala na vitendea kazi.

4. Uratibu wa afya mazingira.

5. Uratibu wa Tiba.